DC GAIRO AAGIZA WACHIMBAJI MADINI WASIO NA LESENI KUSIMAMISHA UCHIMBAJI MARA MOJA


Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe akiwa na kamati ya Ulinzi na Usalama mara baada ya kutembelea sehemu ya migodi inayochimbwa kinyemela na wachimbaji wasiokuwa na leseni.

Moja ya mashine zilizokutwa eneo la mgodi.

Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe amesikitishwa na makampuni ya uchimbaji madini ya viwandani wanaochimba madini mbalimbali Wilayani hapo hasa aina ya Felispar bila leseni.

Mhe. Mchembe aliyasema hayo alipotembelea migodi ya Kata ya Rubeho ambapo wachimbaji wameweka mashine nzito na wanafanya kazi wakati hawana leseni.

Sheria ya Madini ya mwaka 2010, kifungu cha 18 kimeweka bayana adhabu kwa mchimbaji haramu. Ikiwa ni mtu binafsi faini isiyozidi milioni 5 au kifungo miaka mitatu au vyote pamoja. Kama ni kampuni basi ni faini isiyozidi shilingi milioni 50.

Mheshimiwa Mchembe aliendelea mbali na kuelezea kifungu cha 6 (4) cha Sheria ya Uwazi na Uwajibikaji namba 29 ambapo madini yaliyopatikana kupitia uchimbaji haramu yatataifishwa na Serikali chini ya Kamishna wa madini na kuuzwa kwa mnada. Mitambo yote pia inapaswa kutaifishwa.

Akiambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya Mhe. Mchembe ametoa maagizo hayo na kumtaka Afisa Madini Mkoa na Kanda kufatilia jambo hilo kwa karibu.

Pia amepiga marufuku raia wa kigeni kutembelea maeneo ya machimbo bila kibali. Aidha uzingatiwaji wa kanuni 3 (1) (2) ambapo mchimbaji anatakiwa kuwasilisha kwa Afisa Madini mkazi kanda taarifa ya tathmini na mpango wake wa utunzaji wa mazingira kabla ya kuanza kuchimba madini.

Wilaya ya Gairo ina madini aina mbalimbali na maeneo ya milimani yameachwa na mashimo makubwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527