COCA-COLA BONITE YAZIDI KULETA RAHA YA MZUKA WA SOKA NA COKA KANDA YA KASKAZINI



Washindi wa luninga na pikipiki wakifurahia zawadi zao.
Washindi wa luninga na pikipiki wakifurahia zawadi zao.
Mmoja wa washindi wa fedha taslimu akipokea zawadi yake
Wakati mashindano ya kombe la Dunia 2018 yanakaribia, kampuni ya Coca-Cola Bonite Bottlers Limited ya mjini Moshi inazidi kumwaga zawadi za pikipiki,luninga za kisasa na fedha taslimu kwa wakazi wa Kanda ya Kaskazini kupitia promosheni ya Mzuka wa Soka na Coka inayoendelea.

Akiongea katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi 16 wa wiki liyopita, Meneja Mauzo wa Bonite, mkoa wa Arusha Bw. Boniphace Mwasi, alisema zaidi ya wateja 50 wamejishindia zawadi na zawadi bado ziko nyingi. “Bado tunazo zawadi nyingi hivyo natoa wito kwa wakazi wote wa kanda ya kaskazini kuchangamkia kunywa soda za Coca-Cola, ili waweze kujishindia zawadi”.

Wakiongea muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi zao washindi waliishukuru kampuni ya Coca-Cola kwa kubuni promosheni zenye mwelekeo wa kuleta furaha kwa jamii hususani kwa kuwakwamua kiuchumi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527