WAZIRI AMTUMBUA MENEJA KITENGO CHA BAHARI


Meneja kitengo cha bahari na maeneo tengefu, Dk Milali Machumu 
***
Meneja kitengo cha bahari na maeneo tengefu, Dk Milali Machumu amesimamishwa kazi ikielezwa kuwa ameshindwa kukisimamia ipasavyo.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amesema mbali na kumsimamisha kazi, amevunja bodi ya wadhamini ya kitengo hicho na ameagiza Dk Machumu achunguzwe.

Mpina amesema hayo leo Jumatatu Aprili 16, 2018 alipozungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma akitoa ufafanuzi wa kasoro zilizoainishwa katika taarifa ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2016/17 zinazohusu wizara hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527