Monday, April 16, 2018

UKUTA WAUA DAR

  Malunde       Monday, April 16, 2018
Mtoto mmoja aliyefahamika kwa jina la Nasra Ally (9) amefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa baada ya kuangukiwa na ukuta usiku wa kuamkia leo Jumatatu, Aprili 16.Tukio hilo limetokea katika Mtaa wa Kinzinga pembezoni mwa mto Kizinga kata ya Kijichi jijini Dar es Salaam.


Diwani wa kata hiyo Eliasa Mtalawanje amesema Nasra na wenzake walihifadhiwa katika nyumba hiyo kutokana na nyumba za wazazi wao kujaa maji yaliyotokana na mvua zinazoendelea kunyesha.


Amesema hadi sasa nyumba 50 zimejaa maji hali iliyosababisha wengine kulala nje wakilinda mali zao.


"Vitu vingine wamefanikiwa kuviokoa lakini vingine vimeharibika, mimi naomba wawe wavumilivu hasa katika kipindi hiki na waishi kwa tahadhari zaidi," amesema.


Baba mzazi wa marehemu Ally Abeid amesema walisikia kishindo kikubwa huku baadhi ya kinamama kupiga kelele kuashiria kwamba kuna hatari.


"Sisi tulikuwa huku bondeni, kwa sababu tangu juzi tunalala nje, tulivyofika tulikuta ukuta umebomoka na watoto sita wakiwa nje lakini kati yao wa kwangu hakuwepo," amesema huku akinyoosha mikono kumshukuru Mungu.


Amesema kwa sasa mwili umepelekwa katika hospitali ya Temeke na taratibu za mazishi zinaendelea.
Na Asna Kaniki, Mwananchi
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post