MWENGE WA UHURU WATUA KIGOMA...RC MAGANGA ATAKA UTUMIKE KURUDISHA WAKIMBIZI KWAO


Mwenge wa uhuru umewasili mkoa wa Kigoma ukitokea mkoani Kagera ambapo unatarajiwa kuzindua , kutembelea na kuweka mawe ya msingi katika miradi 50 yenye tamani ya shilingi bilioni 12.6 katika miundombinu ya maji,afya, elimu.

Akipokea Mwenge huo leo mkuu wa mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali mstaafu, Emanuel Maganga kutoka kwa Mkuu mkoa wa Kagera katika kijiji cha Nyamtukuza wilaya ya Kakonko alisema mwenge huo utakimbizwa katika halmashauri nane na utaanza kukimbizwa katika wilaya hiyo na kumuomba kiongozi wa mbio za mwenge Charles Kabeho mwenge huo utumike kuhimiza wakimbizi walioko Tanzania kurejea nchini kwao kwa hiyari kwa kuwa nchi hiyo kwa sasa ina amani na ni tulivu.

Hata hivyo mkuu huyo ameahidi kuhakikisha wanafanyia kazi changamoto zote zitakazojitokeza katika mradi wowote na kuomba wananchi wajitokeze kwa wingi kuupokea mwenge huo, na mwenge huo uwe chachu ya kufufua ubadhirifu na kuchochea wananchi kujitolea kuchangia miradi na watumishi kufanya kazi kwa uadilifu kwa kuwa Mwenge wa uhuru ni nguzo kuu iliyoachwa na Baba wa taifa unatakiwa kuenziwa na watu wote.

Akipokea Mwenge huo Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala alisema katika wilaya hiyo Mwenge utazindua na kutembelea miradi 5 yenye thamani ya shilingi 552,199,651.00 ukiwemo mradi wa kituo cha afya cha Nyanzige wenye thamani ya shilingi 271,299,651; mradi wa maji kijiji cha kasanda tsh 227,000,000.00;Jengo la kitega uchumi kasanda 20,000,000.00, vyumba vitatu vya madarasa shule ya msingi Mugamza shilingi 33,900,000.00 na uzinduzi wa klabu ya wapinga rushwa shule ya msingi Kinonko.

Aidha Mkuu huyo alisema miradi hiyo itawasaidia sana wananchi wa wilaya hiyo kwa kuwa ni kipindi kirefu sana wananchi wamekuwa wakitumia wodi moja wanawake na watoto na baada ya kituo hicho cha afya kukabidhiwa na wananchi na kuanza kutumika na kupatikana huduma hizo.

Akitoa ujumbe wa Mwenge Kiongozi wa Mbio za mwenge, Charels Kabeho alisema ujumbe wa Mwenge mwaka huu ni elimu ni ufunguo wa maisha wekeza sasa kwa maendeleo ya Taifa letu na pamoja na kauli mbiu hiyo mbio za mwenge wa uhuru zitaendelea kuhamasisha jamii kupambana na rushwa , mapambano dhidi ya ukimwi na mapambano dhidi ya malaria na mapambano dhidi ya madawa ya kulevya.

Akizindua Kituo cha Afya Nyanzige katika kijiji cha Nyanzige alisema jengo hilo limetumia fedha nyingi sana za serikali na kuomba wananchi kuendelea kutumia kituo hicho kuhakikisha wanatumia hospitali hiyo kupima afya zao na kuhakikisha wanapiga vita maambukizi ya Malaria na Ukimwi.

Na Rhoda Ezekiel - Malunde1 blog
Kiongozi wa Mbio za mwenge, Charels Kabeho akizungumza wakati mkoa  wa Kagera ukikabidhi mwenge huo mkoani Kigoma- Picha zote na Rhoda Ezekiel- Malunde1 blog
Kulia ni mkuu wa mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali mstaafu, Emanuel Maganga akikabidhi mwenge kwa Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala(kushoto)



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527