Saturday, April 21, 2018

WAHANDISI WATAKIWA KUZINGATIA RAMANI ZA MIRADI YA SERIKALI

  Malunde       Saturday, April 21, 2018

Kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa, Charles Kabeho amewaagiza Wahandisi wa Halmashauri kusimamia na kuzingatia mpangilio uliowekwa katika ramani ya majengo ya miradi ya Serikali, inayojengwa kwa kutumia fedha za ndani ili kuhakikisha majengo yanayojengwa yanakuwa ni yenye ubora na yanayodumu muda mrefu.

Rai hiyo aliitoa jana  katika kijiji cha Kalinzi kata ya Kalinzi wilaya ya Kigoma Vijijini mkoani Kigoma baada ya kutembelea jengo la kituo cha afya na kubaini ujenzi huo haujazingatia vigezo vya serikali na umejengwa chini ya kiwango.

 Hali hiyo ilisababisha kiongozi huyo kukataa kuweka jiwe la msingi katika mradi huo unao tarajiwa kujengwa kwa kiasi cha shilingi milioni78, na kuwahudumia zaidi ya wananchi elfu 27 wa kata ya Kalinzi.


Kiongozi huyo alisema Mhandisi wa halmashauri ya wilaya ya Kigoma Ujiji ametumia nondo nne katika jengo ambalo lilihitajika kuwekewa nondo nane kutokana na sababu zake binafsi na ujenzi wa jengo hilo lilitakiwa kuzingatia ujenzi huo na kupelekea kukataa kuweka jiwe la msingi katika mradi wa kituo cha afya na kutoa msisitizo kwa wahandisi kufuata maelekezo ya mradi na kuomba ushauri kwa wahandisi wengine ili kuweza kujenga majengo yenye ubora.


"Unaweza kuona ramani ina mapungufu niwashauri wahandisi jitahidini kuuliza kwa wahandisi wengine ili muweze kujenga majengo yenye ubora na ya kudumu muda mrefu hatakama jengo lako nyumbani huwezi kujenga kwa kutumia nondo tatu kutokana na mzigo uliobebwa na jengo hili Mhandisi hujatendea haki jengo hili simaanishi tusipo weka jiwe la msingi halitaendelea au watu hawatapata huduma, hapana hili ni fundisho kufuatilia viwango vinavyohitajika.

"Niombe Mkuu wa wilaya ulisimamie hili, sisi kama Mwenge wa Uhuru tumeonelea uwekaji wa jiwe la msingi halitawekwa na mwenge wa uhuru litawekwa kwa utaratibu mwingine", alisema Kiongozi wa Mbio za Mwenge.


Kwa upande wake Mhandisi wa Halmashauri ya wilaya ya Kigoma Vijijini, Michael Ntambala alisema yeye kama mhandisi mshauri wa mradi huo atahakikisha anasimamia mradi huo marekebisho yote yaliyotolewa na viongozi wa mbio za mwenge na kwamba walitumia nondo nne kwa kuwa jengo walilojenga halina uzito mkubwa na kwamba atashirikiana na wahandisi wengine kuona suala hilo wanalitatua.

Nao baadhi ya wananchi kata ya Kalinzi walisema Kituo hicho cha Afya kimejengwa kwa nguvu za wananchi na wamekuwa wakijitolea sana na serikali ilichangia fedha na hela nyingine zilitoka kwa Wafadhili na wao kama wananchi wanatamani sana kuona mradi huo umekamilika na kuushukuru mwenge wa uhuru kupita na kuibua mapungufu yaliyopo katika miradi hiyo na kwamba anahakika mradi huo utarekwbishwa kutokana na maelekezo.

Walisema wananchi hawana uelewa mkubwa wala utaalamu wa kufanya miradi inayotekelezwa na serikali na kuwaomba wahandisi kusimamia maelekezo yanayotolewa katika miradi ilikuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati na kutumia mafundi ambao watajenga majengo yenye ubora na wananchi waendelee kupata huduma karibu.

Na Rhoda Ezekiel - Malunde1 blog

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post