WABUNGE WALIOTISHIWA UHAI WATAKIWA KURIPOTI POLISI

Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson amemtaka Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche (Chadema) na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT- Wazalendo) kwenda kuripoti polisi taarifa zao za kutishiwa uhai.


Pia amemuagiza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba kufuatilia kwa karibu taarifa hizo za wabunge kutishiwa uhai.


Agizo hilo la Naibu Spika limetolewa leo bungeni mjini Dodoma wakati akitolea ufafanuzi mwongozo wa Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema) aliyeiomba serikali itoe maelezo kuhusu taarifa za wabunge hao kutishiwa uhai.


Waitara amesema licha ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kusema wabunge wako salama, taarifa zilizopo kwenye vyombo vya habari ni kwamba wabunge hao wamesema wanafuatiliwa na watu wanaowatishia uhai hivyo wakapewa nafasi ndani ya bungeni kuelezea taarifa hizo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527