Monday, April 16, 2018

MWENYEKITI WA CHADEMA ATUMBULIWA KWA KUKIUKA KATIBA

  Malunde       Monday, April 16, 2018
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia baraza kuu la uongozi Mkoa wa Morogoro limemvua James Mkude nafasi aliyekuwa akiishika ya Mwenyekiti wa Manispaa ya Morogoro kutokana na tuhuma za kujihusisha na matukio yaliyo kinyume na katiba ya chama hicho.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa chama hicho mkoani humo ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mlimba Bi. Suzani Kiwanga na kusema hatua hiyo imekuja baada ya kujiridhisha na tuhuma zilizo wasilishwa ndani ya chama hicho ingawa ni tuhuma binafsi zinazomkabili mwenyekiti huyo aliyesimamishwa na kwamba hazihusiani na chama.

Akitoa maadhimio ya wajumbe wa baraza la uongozi la chama hicho mkoa wa Morogoro waliokutana kujadili muenendo wa mwenyekiti huyo, Bi. Suzani amesema kuwa kwa mujibu wa katiba ya chama hicho ya mwaka 2006 toleo la mwaka 2016 kifungu cha saba pamoja na maadili ya uongozi kinatoa mamlaka kwa baraza hilo kumsimamisha mtu yeyote atakae kiuka maadili ya kinidhamu ya chama hicho.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post