SERIKALI YAPIGA MARUFUKU UAGIZAJI WA MITA ZA LUKU ZA UMEME NJE YA NCHI

Waziri wa Nishati, Dr. Medard Kalemani amesema kuanzia Julai 1,2018 serikali itasitisha rasmi uagiziaji wa mita za Luku za umeme kutoka nje ya nchi ili kutoa fursa kwa wawekezaji wa ndani.


Dr. Kalemani ameyasema hayo wakati akizindua kiwanda cha kutengenezea mashine za Luku maeneo ya Mbezi, ambapo amesema uwepo wa wawekezaji wa ndani utaokoa muda na kupunguza gharama hasa katika sekta hiyo ya nishati.


Amesema kuwa usitishwaji huo ulitanguliwa na ule wa awali ambapo walisitisha uingizaji wa nguzo za umeme kutoka Afrika Kusini na Transformer kutoka India.


Amesema kuwa kuna faida nyingi kwa Mita hizo kutengenezwa nchi ikiwemo kuokoa muda wa uagiziaji na kupunguza gharama.


“June 2017 tulisitisha rasmi uingizaji wa nguzo kutoka Afrika Kusini, ambapo nguzo moja tulikuwa tunanunua Laki 3 hadi Laki 4, wakati ukinunua nguzo za hapa ndani ni Laki 2” amesema Kalemani


” Shirika la Tanesco limekuwa na mizigo mikubwa kwa sababu ya gharama ya kuagizia vifaa kutoka nje ya nchi,”-Kalemani


Pia Dr. Kalemani amesema kuna tatizo la ubora, kwani kuna baadhi ya nchi zina majina makubwa lakini bidhaa zao feki, kwani mwaka jana ziliungua transformer 100 kutoka India kwa wakati mmoja.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527