Thursday, April 5, 2018

Picha: BASI LA CITY BOYS LAGONGANA NA LORI NA KUUA WATU 12,KUJERUHI ZAIDI YA 40 TABORA

  Malunde       Thursday, April 5, 2018
Watu 12 wamepoteza maisha na wengine 46 kujeruhiwa baada ya basi la City Boys lililokuwa linatoka Karagwe kwenda Dar es salaam kugongana na lori katika eneo la Makomero wilaya ya  Igunga mkoa wa Tabora. 

Ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo Alhamisi Aprili 4,2018.

Inaelezwa kuwa gari lenye namba za usajili T486 ARB Fuso likiwa na mzigo wa viazi likitokea Singida kuelekea Igunga lilipasuka tairi ya kulia  na kutumbukia katika mashimo mawili barabarani na kukosa uelekeo na kugonga basi la abiria T983 DCE Scania kampuni ya City Boys.

 Chanzo cha habari cha Malunde1 blog kinasema watu 10 walifariki katika eneo la tukiona wawili wakiwa wanapelekwa hospitali ya wilaya ya Igunga. 

Aidha majeruhi 46 wamefikishwa katika hospitali ya Igunga kwa matibabu  kati yao watatu ni mahututi na wawili wamepelekwa hospitali ya rufaa ya Bugando na amepelekwa hospitali ya Nkinga.

Dereva wa basi pia alipoteza maisha  papo hapo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Wilbroad Mutafungwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba atatoa taarifa rasmi baadae.
Na Kadama  Malunde - Malunde1 blog
Muonekano wa basi la City Boys baada ya ajali

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post