Monday, April 23, 2018

MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI AJIUA BAADA YA KUBAINI ANAISHI NA VVU SHINYANGA

  Malunde       Monday, April 23, 2018

Mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Mwasele iliyopo katika manispaa ya Shinyanga Happiness William (18) amefariki dunia kwa kujinyonga kwa kwa kutumia kamba kutokana na msongo wa mawazo baada ya kubaini kuwa anaishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU). 

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari ya kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Simon Haule tukio hilo limetokea jana Aprili 22,2018 majira ya saa 12 na dakika 40 jioni. 

Alisema mwanafunzi huyo,mkazi wa Kambarage mjini Shinyanga aligundulika akiwa amefariki baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba aliyoifunga kwenye paa la nyumba aliyokuwa anaishi na wazazi wake. 

“Chanzo cha tukio ni msongo wa mawazo baada ya kugundua kuwa anaishi na maambukizi ya VVU,mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi wa daktari na kukabidhiwa kwa ndugu zake kwa ajili ya mazishi”,alieleza Kamanda Haule. 

Aidha alitoa wito kwa wazazi,walezi na wananchi kwa ujumla kuwa karibu na watoto na vijana ili kujua shida na changamoto zinazowakabili ili kuchukua hatua za kuwashauri na kuwatia moyo wa matumaini pale wanapokata tamaa ya maisha. 

Na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post