MWANAFUNZI WA DARASA LA TATU AFARIKI BAADA YA KUTUMBUKIA KWENYE KARO LA MAJI TAKA KAHAMA


Mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi Nyahanga wilayani Kahama mkoani Shinyanga Daniel Yohana Maziku (09) amefariki dunia baada ya kutumbukia kwenye karo la maji taka. 

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Simon Haule amesema tukio hilo limetokea jana Jumapili Aprili 22,2018 majira ya saa tano asubuhi katika mtaa na kata ya Mhungula tarafa ya Kahama Mjini. 

“Mwanafunzi huyo aligundulika akiwa amefariki baada ya kutumbukia kwenye karo la maji taka jirani na makazi yao katika mtaa wa Mhungula,chanzo ni mtoto huyo kucheza jirani ya karo hilo na kutumbukia humo baada ya kuteleza”,ameeleza Kamanda Haule. 

Na Kadama Malunde – Malunde1 blog

Theme images by rion819. Powered by Blogger.