MRITHI WA LWANDAMINA ' MKONGOMANI' ATUA BONGO


Huyu ndiyo kocha mpya wa Yanga.

Kocha mwenye asili ya Kongo, Zahera Mwinyi 'Mkongoman' ametua katika ardhi ya Tanzania, Jijini Dar es Salaam leo hii kwa lengo la kwenda kujiunga na Klabu ya Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga.


Hayo yamebainishwa na taarifa rasmi zilizotolewa mchana huu kutoka kwa uongozi wa Yanga kupitia ukurasa wao maalum wa kijamii ambapo wameonekana kuwa na furaha ya ujio wa kocha huyo mpya na kujigamba kwamba amekuja kuiangazamiza Simba katika mchezo wao wa watani wa jadi mnamo Aprili 29, 2018.

"Kocha Zahera Mwinyi 'Mkongoman' mwenye uraia wa Ufaransa, tayari ametua nchini", imesema taarifa hiyo.


Ujio wa kocha huyo ni wazi kabisa kuwa timu Yanga imebwagana na kocha wake, George Lwandamina aliyeondoka majuma mawili yaliyopita na kurejea kwao Zambia ambapo taarifa zaidi zinadai ameenda kukamilisha mipango yake ya kujiunga na klabu yake ya zamani, Zesco United. 

Lwandamina alifanikiwa kujiunga na Yanga mwezi wa 11 mwaka 2016 ambapo alichukua nafasi ya Mholanzi, Hans van der Pluijm na katika kipindi hicho ameiongoza timu katika michezo 77 ya mashindano yote akitoa sare 18, kushinda 45 kati ya hizo mbili kwa penati baada ya sare ndani ya muda wa kawaida na kufungwa 14, tano kwa penati baada ya sare katika muda wa kawaida.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.