Tuesday, April 3, 2018

KESI YA MBOWE NA WENZAKE KUUNGURUMA APRILI 16

  Malunde       Tuesday, April 3, 2018
Upande wa mashtaka wa kesi inayowakabili viongozi saba wa Chadema, akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iruhusu kesi hiyo isikilizwe kwa haraka, ikiwezekana jambo hilo kuanza kesho.


Wakili huyo wa Serikali, Faraja Nchimbi amesema msingi wa maombi hayo ni kutokana nai upelelezi kukamilika.


Amesema sababu nyingine ni kwamba washtakiwa wengi katika kesi hiyo ni wabunge na kwa kuwa kesi hiyo inavuta watu wengi ni vema ikasikilizwa haraka.


"Kwa hiyo tunaomba kama ikiwezekana kesho mchana tuendelee na usikilizaji wa awali ili sisi upande wa mashtaka tuweze kuwasilisha kile tulicho nacho,” amesema Nchimbi.


Hata hivyo, wakili wa upande wa utetezi, Peter Kibatala amepinga mapendekezo hayo akieleza kuwa ndiyo kiongozi wa jopo la mawakili wa utetezi, kesho atakuwa na kesi nyingine Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi na kesho kutwa pia atakuwa na kesi nyingine.


Amesema Aprili watakuwa na semina za mawakili ambazo ni za lazima kwa kuwa bila kupata alama zinazohitajika kutokana na semina hizo, leseni yake haiwezi kuhuishwa.


Vilevile, amesema kuanzia Aprili 13 watakuwa na mkutano wa mawakili wote jijini Arusha na akapendekeza usikilizwaji wa awali wa kesi hiyo ufanyike Aprili 16.


Katika uamuzi wake, Hakimu Wilbard Mashauri amekubaliana na mapendekezo ya upande wa utetezi na akaamuru usikilizwaji wa awali ufanyike April 16, 2018.


Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi tarehe hiyo, itakapoitwa kwa ajili ya usikilizwaji wa awali.


Mbali ya Mbowe viongozi wengine walioachiwa kwa dhamana ni Katibu Mkuu Dk Vicent Mashinji, Manaibu Katibu Wakuu John Mnyika (Bara), Salum Mwalimu (Zanzibar), Mbunge wa Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa, Mweka Hazina wa Baraza la Wanawake wa chama hicho Ester Matiku na mwenyekiti wa baraza hilo, Halima Mdee.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post