Sunday, April 1, 2018

HII NDIYO WILAYA YENYE IDADI KUBWA YA MAKAHABA...DANGURO KUBWA ZAIDI LABORESHWA

  Malunde       Sunday, April 1, 2018
Wasanii wa michoro wasiokubali jinsia ya maumbile yao wamekuwa wakiipatia sura mpya ya michoro ya rangi za kuvutia wilaya yenye idadi kubwa ya makahaba ya Sonagachi iliyopo katika jiji lililopo mashariki mwa India la Kolkata (zamani likiitwa Calcutta).

Ikisemekana kuwa wilaya yenye idadi kubwa zaidi ya mahahaba bara Asia, Sonagachi ni wilaya yenye mitaa yenye barabara nyingi nyembamba na njia za uchochoroni kati kati mwa jiji la Kolkata, ikiwa ni makazi ya makahaba takriban 11,000.

Wakifanya kazi kwa ushirikiano na wasanii wenye makao yao Bangalore, wasanii wa michoro wasiokubali maumbile yao ya jinsia (transgender) walichora michoro kwenye michoro ya rangi za kuvutia kwenye baadhi ya majengo kama sehemu ya kampeni ya kuhamasisha umma kuhusu haki za makahaba na pia kujaribu kuzuia unyanyasaji dhidi ya wanawake.

Uchoroji wa michoro hii ulichukua muda wa wiki nzima

Mengi kati ya madanguro haya yamechakaa

Kuta katika mtaa wenye majengo yaliyosongamana pia zilipakwa rangi.
Kuna mipango ya kuyapaka rangi majengo zaidi katika wilaya ya Sonangachi.

Ukahaba umesalia kuwa tatizo kubwa kwa India, ambako wanawake milioni tatu wanaaminiwa kufanya biashara ya ukahaba.


Picha ya jengo lenye mchoro katika mtaa wa Sonangachi wa makahaba katika wilaya ya Kolkata.

Picha hiyo inaonyesha mchoro uliochorwa kwenye jengo la chama cha ushirika cha makahaba.

Hapa wapitanjia na wafanyabiashara wanaonekana kwenye moja ya jengo lililopigwa rangi.
.Wapita njia wa Kihindi wakipita kwenye mtaa wa madanguro ya makahaba yenye michoro katika wilaya ya Sonangachi jijini Kolkata

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post