FERGUSON AMPA ZAWADI WENGER, AAGA KWA KIPIGO | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, April 29, 2018

FERGUSON AMPA ZAWADI WENGER, AAGA KWA KIPIGO

  Malunde       Sunday, April 29, 2018
Kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson leo amemuaga kocha wa Arsenal Arsene Wenger kwa kumpa zawadi maalum kabla ya mechi ya ligi kuu iliyomalizika kwa kufungwa 2-1 usiku huu kuanza.

Fergusona amemkabidhi zawadi hiyo kwa niaba ya klabu ya Manchester United ikiwa ni sehemu ya kutambua mambo mbalimbali ambayo Wenger ameyafanya kwenye ligi kuu ya soka ya England EPL.

Wenger ametangaza rasmi kuachana na Arsenal aliyoifundisha kwa miaka 22 mwishoni mwa msimu huu. Hata hivyo Wenger bado hajaweka wazi kama atastaafu au atakwenda kufundisha timu nyingine.
Katika mchezo uliopigwa jioni hii kwenye uwanja wa Old Trafford, Wenger ameshinwa kulinda heshima ya kutofunga baada ya vijana wake kuruhusu bao la dakika za mwisho kutoka kwa Marouane Fellaini.

Mabao ya Man United yamefungwa dakika ya 16 na kiungo Paul Pogba na dakika ya 90 na Marouane Fellaini huku lile la Arsenal likifungwa na Henrikh Mikhtaryan dakika ya 51. Wenger na Mourinho sasa wamekutana mara 13 na Mourinho ameshinda mara 8 na kutoka sare mara 5.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post