Wednesday, April 25, 2018

ALIYEPIGWA BOMU KWENYE UUME APANDIKIZIWA UUME NA KORODANI ZINGINE

  Malunde       Wednesday, April 25, 2018
Jopo la madaktari katika chuo kikuu cha Johns Hopkins waliomfanyia upandikizaji wa uume
**
Jopo la madaktari wamefanikiwa kufanya upandikizaji wa kwanza wa uume na korodani.

Upasuaji huo waliomfanyia askari alijeruhiwa na bomu huko Afghanistan katika chuo cha Johns Hopkins mjini Baltimore, Maryland,

Madaktari hao walitumia uume na korodani zilizoondolewa kwa watu waliokufa.

Madaktari hao wamesema askari huyo atarudishiwa uwezo wa kufanya mapenzi ,jambo ambalo sio rahisi kama mtu akifanyiwa upasuaji wa uume.

Upasuaji huo umefanyiwa upasuaji mara nne kumi na moja na upandikizi huu ulitumia masaa kumi na nne tarehe 26 machi mwaka huu.

Huu ni upasuaji wa kwanza kumalizika salama na kurejesha sehemu hizo kurudi kwenye hali yake ya kawaida.

Madaktari wanasema kwamba korodani kutoka kwa mfadhili hazijapandikizwa kutokana na sababu za maadili.

Askari aliyefanyiwa upandikizaji ametaka kutofahamika.

„Nilipoamka nilijisikia kuwa nimerudi kwenye hali yangu ya kawaida,kiukweli niko sawa kwa sasa",Askari huyo alieleza.

Wataalamu wa upasuaji huo wanatarajia kuwa askari huyo atapona ndani ya miezi 6 hadi 12.
Chanzo- BBC
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post