ZITTO KABWE ATOA NENO MAANDAMANO

Kuelekea siku ya kesho April 26, 2018, ambapo Taifa la Tanzania litakuwa linaadhimisha miaka 54 ya Muungano wa iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar, na huku pia fununu za kufanyika maandamano ya Mange Kimambi, zikiwa zimesambaa nchini kote, Mbunge wa Kigoma Mjini, Mhe. Zitto Kabwe, ametoa neno jioni hii.

Akiandika katika ukurasa wake wa Twitter, Mhe. Zitto ameonekana kushangazwa sana na mazoezi ya Jeshi la Polisi yaliyofanyika siku ya leo katika maeneo tofauti tofauti hapa nchini, huku akiyafananisha mazoezi hayo na maandamano, hivyo kujiuliza endapo Jeshi hilo lilipata kibali, kama ambavyo serikali ya Tanzania kupitia kwa viongozi wake imekuwa ikisisitiza.
  1. Leo imekuwa siku ya maandamano ya Polisi. Sijui waliomba kibali?
  2.  
Siku ya leo maeneo tofauti tofauti yameshuhudia Jeshi la Polisi likikifanya mazoezi yake, kitendo ambacho kilikuwa hakijazoeleka kufanyika kwa siku za hapo nyuma, na hivyo kitendo cha leo kujenga hisia kwamba Jeshi hilo linatuma salamu kwa wale wote watakaoandamana siku ya kesho.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.