Thursday, March 1, 2018

"UNA HAKI YA KULAUMU ILI UPUMUE"-NAPE NNAUYE

  mtilah       Thursday, March 1, 2018


Mbunge wa jimbo la Mtama kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Nape Nnauye amefunguka na kudai kutohusika na kupanga mambo mbali mbali yanayoendelea nchini baada ya kutuhumiwa kufanya hilo na mmoja wa raia.

Nape Nnauye amefunguka hayo wakati akijibu moja ya hoja ya mtu aliyemtuhumu yeye kama Mbunge wa CCM na kusema kiongozi huyo anajua na kuona haki za raia zikivurugwa
"Naamini unaitwa Kusiluka,nimesoma lawama zako kwangu,una haki ya kulaumu ili upumue, lakini kuna kikao nimeshiriki kupanga hayo unayonituhumu?! Nadhani kuwa mkweli kwa nafsi yako tuhuma hizo ni nzito si sawa kuzisema bila kuwa na hakika, sihusiki na hayo usemayo na nayalaani pia" Alidai Nape Nnauye

Nape Nnauye aliwataka Watanzania kwa pamoja kuwasha mishumaa ya matumaini na hapo ndipo mtu huyo alipoibuka mwananchi huyo na kusema kuwa kiongozi huyo yeye anatambua na kujua kinachoendelea nchini sasa, jambo ambalo Nape Nnauye amelikana na kusema hata yeye analaani kwa vitendo vinavyoendelea nchini.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post