SIMBA SC KUTUMIA SIKU 3 KUIWINDA AL MASRY

Baada ya kupewa mapumziko ya siku moja, kikosi cha Simba hatimaye jioni ya leo kimeanza rasmi maandalizi ya mchezo wake wa kwanza Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Al Masry.

Kikosi hicho chini ya kocha Mfaransa Pierre Lechantre kilipewa mapumziko ya siku moja baada ya mchezo wake wa ligi kuu dhidi ya Stand United uliomalizika kwa sare ya 3-3 ijumaa jioni.

Taarifa ya klabu hiyo imeeleza kuwa timu hiyo ipo kambini tayari kwa maandalizi ya mchezo huo ikianza na mazoezi ya jioni leo na itafanya hivyo hadi jumanne jioni kisha jumatano kushuka kwenye uwanja wa taifa kukipiga na Wamisri.

''Kikosi cha Simba kimeingia kambini tayari kujiandaa na mchezo dhidi ya Al Masry utakaochezwa siku ya Jumatano saa 12:00 jioni'', imeeleza sehemu ya taarifa.

Simba imetinga hatua ya kwanza ya michuano hiyo baada ya kushinda kwa jumla ya mbao 5-0 kwenye mchezo wa hatua ya awali dhidi ya timu ya Gendarmerie Nationale FC ya Djibouti.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.