MWENYE SHIDA NGUVU ZA KIUME MGONJWA | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, March 22, 2018

MWENYE SHIDA NGUVU ZA KIUME MGONJWA

  Malunde       Thursday, March 22, 2018

Watu wenye nguvu kidogo ya kiume, wanaelezwa kuwa na uwezekano kuugua magonjwa mengine, imebainika. 

Utafiti uliofanyika kwa kuhusisha watu 5,177 umebaini waishio na nguvu kidogo za kiume wana uwezekano wa asilimia 20 kuugua maradhi kadhaa.

Baadhi ya maradhi hayo yanatajwa kuwa ni mafuta mengi mwilini, pia shinikizo la damu, huku wakiwa hatarini kuugua maradhi kama kisukari.

Kutokana na hilo, watafiti wana ushauri kwamba, mtu akibainika na nguvu kidogo za kiume anapaswa kukaguliwa afya yake katika maeneo mengine ya kiafya.

Mwanataaluma Profesa Alberto Ferlin, kutoka Chuo Kikuu cha Bresci, aliyeongoza utafiti huo anasisitiza:"Wanaume hao wako hatarini kupata matatizo mengine ya afya ambayo yanaingiza maishani yake hatarini.”

Mtaalamu Profesa Ferlin, anashauri kila anayekutwa na shida hiyo ya nguvu kidogo ya kiume, afya yake ifuatiliwe kwa karibu.

Mshauri Kevin McEleny kutoka, Uingereza anashauri kuwa katika hali iliyoko Uingereza, katika hali iliyozoeleka nchini Uingereza, watu wenye shida ya nguvu ya kiume hawafuatiliwi sana.
Chanzo- Nipashe
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post