Thursday, March 22, 2018

FATMA KARUME AJITOSA KUMRITHI TUNDU LISSU TLS

  Malunde       Thursday, March 22, 2018
Wakili wa kujitegemea, Fatma Karume amejitosa kumrithi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kwa kugombea urais wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS), utakaofanyika Aprili 14, mwaka huu.


Lissu, ambaye aliteuliwa kugombea nafasi hiyo lakini ameshindwa kukidhi matakwa ya kamati kutokana na fomu ya uteuzi iliyowasilishwa kwa sekretarieti hiyo.


Kwa mujibu wa sheria mpya, Lissu hataweza kugombea tena nafasi hiyo kwani kifungu cha nane cha sheria hiyo, kinamzuia mtu ambaye ni kiongozi wa chama chochote cha siasa, kuongoza chama hicho.


Katika kinyang’anyiro hicho, Fatma atachuana na Godwin Mwapongo, Godfrey Wasonga na Godwin Ngwilimi huku nafasi ya umakamu wa rais ikiwa na mgombea pekee, Rugemeleza Nshalla na Mweka Hazina akiwa Sadock Magai.


Kwa mujibu wa taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uteuzi wa chama hicho, Dk. Kibuta Ongwamuhana, uchaguzi wa rais utatanguliwa na viongozi wa kanda utakaofanyika kila mkoa kuanzia Machi 27, mwaka huu.


Wakizungumzia uchaguzi huo baadhi ya mawakili wamesema wanamtabiria Fatma ushindi wa kishindo kutokana na kuwa na kariba inayofanana na Lissu.


“Fatma atashinda kwa sababu anapenda mtu mwenye ‘tension’ na ni mtu mwenye kujiamini anaweza akaitetemesha serikali na wanasheria wanapenda hivyo,” amesema mawakili wa kujitegemea ambaye hakutaka jina lake litajwe.


Wakili mwingine alisema ingawa sheria hiyo inamkataza Lissu kugombea ambapo walipanga kumchagua tena mwaka huu lakini Fatma anaweza kuziba pengo la Lissu.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post