LORI LAPINDUKA NA KUUA WATU SINGIDA

Jeshi la Polisi mkoani Singida limetoa taarifa juu ya ajali ya moto ambayo imeteketeza lori mapema hii leo, na kusababisha vifo vya watu wawili waliokuwemo kwenye lori hilo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida Debora Magiligimba, amesema ajali hiyo imetokea leo majira ya saa nne asubuhi, baada ya lori hilo kuacha njia na kupinduika na kisha kuwaka moto, na kusababisha vifo vyta dereva na konda wake ambao wote ni wakazi wa Dar es salaam.

“ Lori lenye namba T 167 DQT aina ya flight liner mali ya Petrolmark Afrika ya jijini Dar es salaam, liliacha njia na kupinduka na kisha kuungua, watu waili ambao ni wanaume waliokuwamo wamefariki, uchunguzi wa jeshi la polisi baada ya kupita mzani wa Singida saa 1 asubuhi, gari hiyo ilikuwa inaendeshwa na Erasto Abedi Rusazi na Ramadhani Hashim Ramadhani wote wakazi wa Dar es salaam, na lilikuwa limebeba mafuta”, amesema Kamanda Magiligimba.

Kamanda Magiligimba amesema miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya willaya ya Kiomboi, na ndugu zao wanaombwa kwenda kutambua miili.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.