KIJANA AKUTWA AMEKUFA GESTI


Kijana aliyetajwa kwa jina la Festa Mtunga anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 30 hadi 36 amekutwa amekufa kwenye nyumba ya kulala wageni Chalinze mkoani Pwani.

Hadi sasa haijafahamika kijana huyo ni mkazi wa wapi.

Kamanda wa polisi mkoani Pwani, Jonathan Shana, amewaeleza waandishi wa habari ofisini kwake mjini Kibaha kuwa, tukio hilo lilitokea Machi 27 mwaka huu, saa 4:00 asubuhi huko Chalinze.

Shana amesema Festa alilala kwenye nyumba hiyo lakini ilipofika asubuhi wahudumu walimgongea mlango bila ya mafanikio na ndipo walipotoa taarifa polisi.

"Polisi ilibidi wavunje mlango na kumkuta akiwa amelala peke yake kitandani, hakuwa na jeraha lolote mwilini mwake baada ya uchunguzi na kuondoa mashaka juu ya kifo chake," amesema.

Ametoa wito kwa ndugu wa marehemu kujitokeza kuuchukua mwili huo.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya mkoa ya Tumbi.
IMEANDIKWA NA JOHN GAGARINI - habarileo KIBAHA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527