Friday, March 23, 2018

DIAMOND ATINGA OFISI ZA BASATA KIMYAKIMYA KUYAMALIZA

  mtilah       Friday, March 23, 2018Msanii wa muziki, Diamond Platnumz Ijumaa hii amefanya mazungumzo ya siri na Baraza la Sanaa Taifa ‘Basata’ ikiwa ni siku chache toka aingie kwenye majibizano na Naibu Waziri wa Habari, Juliana Shonza.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo “African Beauty” ametua viwanja vya basata majira ya nchana akiwa na meneja wake, Sallam SK. Hata hivyo baada ya kufanya mazungumzo hakuweza kuzungumza chochote juu ya nini kilitokea.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Basata zinadai muimbaji huyo alifika katika taasisi hiyo ya malezi ya wasanii kwaajili ya kuzungumza na viongozi hao juu ya kauli zake ambazo amekuwa akizitoa juu ya Naibu waziri huyo.

Hata hivyo Basata hawajatoa taarifa yoyote juu ya kikao hicho cha siri ambacho kilichukua masaa kadhaa.

Wadau wa mambo wanadai huwenda muimbaji huyo alikwenda Basata kwaajili ya kuamba radhi juu ya mambo yanayoendelea.

Mapema wiki hii muimbaji huyo wakati anahojiwa na kituo cha redio cha Times FM aliitupia lawama Basata pamoja na Naibu waziri huyo baada ya kufungia nyimbo 15 za wasanii wa bongofleva zikiwemo zake mbili.

Kauli hizo zilimfanya Waziri wa Habari, Dk Mwakyembe kutoa kauli yake na kudai kwamba ameshtushwa na kauli za muimbaji huyo juu ya waziri.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post