TAARIFA KUTOKA IKULU,RAIS MAGUFULI AMEFANYA UTEUZI HUU


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC), Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma na Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Benjamini Mkapa, Dodoma.
Taarifa iliyotolewa leo March 23 , 2018 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Rais Magufuli amemteua Prof. Lazaro S.P. Busagala kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC) kuanzia tarehe 22 March, 2018.
Kabla ya uteuzi huo Prof. Busagala alikuwa Makamu Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kitivo cha Taaluma na Utafiti.
Rais Magufuli amemteua Prof. Damian Gabagambi kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) kuanzia tarehe 22 March, 2018.
Prof. Gabagambi anachukua nafasi ya Mlingi Elisha Mkucha ambaye atapangiwa kazi nyingine. Kabla ya uteuzi huo Prof. Gabagambi alikuwa Mhadhiri wa Uchumi wa Chuo Kikuu cha Kilimo, Sokoine (SUA).
Rais Magufuli amemteua Dkt. Deodatus Michael Mutasiwa kuwa  Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma.
Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Alphone Bilola Chandika kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma. Kabla ya Uteuzi huu Dkt. Chandika alikuwa akikaimu nafasi hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527