Wednesday, March 14, 2018

Breaking : MMILIKI WA MABASI YA SUPER SAMI AKUTWA AMEKUFA MTONI,..INATISHA ANGALIA PICHA

  Malunde       Wednesday, March 14, 2018

Mwili wa mmiliki wa mabasi ya Super Sami, Samson Josiah ulivyokutwa mtoni ukiwa umefungwa kwenye mfuko wa sandarusi na turubai
Mmiliki wa mabasi ya Super Sami, Samson Josiah enzi za uhai wake


Mwili wa mmiliki wa mabasi ya Super Sami Samson Josiah umekutwa ukiwa unaelea kwenye mto Rubana ambao ndiyo mpaka unaotenganisha wilaya za Busega mkoani Simiyu na Bunda mkoani Mara.

Taarifa kutoka vyanzo vya habari vya Malunde1 blog ni kwamba mwili wa Samson Josiah umekutwa ukielea katika mto huo ukiwa umefungwa kwenye mfuko wa sandarusi na turubai leo Jumatano Machi 14,2018 majira ya saa 10 jioni.


Miongoni mwa habari zilizoteka vyombo vya habari Tanzania tangu Machi 9, 2018 hadi ni kuhusu kupotea kwa mmiliki wa mabasi ya Super Sami, Samson Josiah kwa zaidi ya wiki mbili sasa.

Mapema ilielezwa kuwa gari yake ndogo aliyokuwa akiitumia aina ya Toyota LandCruiser ilikutwa imechomwa moto katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti iliyoko mkoani Mara siku ya Machi 9, lakini yeye mwenyewe alikuwa hajapatikana.

Kwa mujibu wa familia ya Bwana Josiah, ambayo inaishi mkoani Mwanza, ilidai kuwa siku ya kupotea kwa Josiah ambayo ni February 27, majira ya usiku, Josiah alimpigia simu mkewe na kumwambia kuwa atarudi nyumbani na mgeni, na hayo yakawa mawasiliano yao ya mwisho.

Mabasi ya Super Sami yanafanya safari zake kuanzia mkoa wa Mwanza, kwenda mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Iringa pamoja na Kagera.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post