WAHUNI WAMSHAMBULIA MAKAMU WA RAIS MSTAAFU


Kiongozi wa Chama cha Wananchi (NPP) Joice Mujuru mapema Alhamisi aliondolewa na kukimbizwa haraka ili kuokoa maisha yake baada ya kundi la vijana waporaji kumshambulia eneo la Glen Norah, wasaidizi wake wamedai.

Katika taarifa fupi, Katibu mkuu wa NPP Gift Nyandoro alisema vijana walinzi wa chama hicho walimlinda makamu huyo wa zamani wa rais.

“Rais wa NPP, Dk Joice Mujuru amepona kushambuliwa aliporushiwa mawe mfululizo aliyorushiwa na vijana wa Zanu PF waliolipwa katika eneo la maduka la Chitubu leo hii Februari 1, 2018,” alisema Nyandoro.

"Tunamshukuru vijana wa NPP ambao walisimama imara kwa ajili ya kumlinda mama Zimbabwe," alisema Nyandoro.

Mwanaharakati wa APP ambaye alizungumza na gazeti la New Zimbabwe kwa simu vilevile alithibitisha kwamba vurugu zilimzuia Mujuru kufanya ziara kwenye kitongoji kikubwa cha nje kidogo ya mji.

"Hali ilikuwa ya kutisha. Wahuni walikuwa wamepakiwa kwenye basi dogo la kukodiwa kutoka Machipisa. Bado haijafahamika kama kuna yeyote aliyejeruhiwa,” alisema.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.