DIWANI WA CHADEMA AJIUZULU NA KUJIUNGA CCM
Diwani wa Hayderer (Chadema) wilayani Mbulu mkoani Manyara, Justin Masuja amejiuzulu nafasi hiyo na kujiunga na CCM.

Masuja amejiunga na CCM leo Februari 12,2018 katika ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti.

Katika mkutano wa hadhara, Mnyeti aliwataka madiwani wa upinzani kuhamia chama tawala ili watekeleze ilani ya CCM ambayo ndiyo ipo madarakani.

Diwani huyo amesema anajiunga na CCM ikiwa ni hatua ya kuunga mkono jitihada za Rais John Magufuli katika kuwatumikia wananchi.

Na Joseph Lyimo, Mwananchi
Theme images by rion819. Powered by Blogger.