Tarime Tena !! KATIBU WA CHADEMA AJIONDOA CHADEMA NA KUHAMIA CCM




Katibu wa Chadema wilaya ya Tarime Mkoani Mara,Elias Thobias Ghati, amehama chama na kutimukia CCM leo Jumatatu Januari 8,2018.

Ghati anakuwa kiongozi wa pili wa chama hicho kutimukia CCM baada ya Zakayo Chacha Wangwe,aliyekuwa Diwani wa kata ya Turwa Wilayani Tarime kufikia uamuzi huo Januari 5,2018.

Ghati amesema kuwa hakushinikizwa na mtu yeyote kuhamia chama hicho, bali ni kwa utashi wake mwenyewe.

Wengine waliohamia Chadema ni mlinzi wa mbunge wa Tarime mjini Emmanuel Ngese na Lucas Marwa ambaye ni mwanachama wa kawaida.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527