SPIKA AAGIZA OLE SENDEKA AHOJIWE KWA KUKEJELI NA KUDHARAU BUNGE







Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka anatakiwa kujitetea mbele ya Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka kuhusu kauli zake zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kwa kile kinachodaiwa kuwa zinakejeli na kudharau Bunge.


Taarifa kutoka Ofisi ya Spika wa Bunge iliyotolewa leo Jumanne inaeleza kuwa Spika Job Ndugai ametoa maelekezo kwa kamati hiyo kumchunguza mbunge huyo wa zamani wa jimbo la Simanjiro.


Katika taarifa hiyo inaelezwa kuwa Spika amechukua hatua hiyo kufuatia kauli zinazonukuliwa katika mitandao ya kijamii kwa lugha za kimasai, kiswahili na kiingereza zikiashiria kejeli na dharau kwa Bunge.


Spika ameitaka kamati hiyo kumuita mkuu huyo wa mkoa, kumhoji na kubaini ukweli na dhamira ya kauli hizo na kutoa mapendekezo kuhusu hatua zinazopaswa kuchukuliwa na Bunge.


Na Ephrahim Bahemu, Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527