Wednesday, January 24, 2018

Picha & Video : MAJAMBAZI YAVAMIA DIDIA SHINYANGA..YAUA,KUJERUHI NA KUPORA FEDHA

  Malunde       Wednesday, January 24, 2018

Mwanaume aliyejulikana kwa jina la Edward Ndonho (32) ambaye ni afisa kilimo kata ya Bukene - Didia wilaya ya Shinyanga Vijijini ameuawa kwa kupigwa risasi na majambazi waliokuwa wanavamia duka la Juma Mnyesi (47) katika kijiji na kata ya Didia wilayani humo.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule aliyefika eneo la tukio,amesema mauaji hayo yametokea jana Januari 23,2018 saa mbili na dakika 40 usiku katika kijiji cha Didia, kata ya Didia, tarafa ya Itwangi, wilaya ya Shinyanga vijijini na mkoa wa Shinyanga.

Kamanda Haule amesema afisa kilimo huyo wa kata ya Bukene - Didia aliuawa kwa kupigwa na risasi ya bunduki aina ya AK 47/SAR sehemu za paji la uso na kisha kutokea kisogoni na kutokwa na damu nyingi na kusababisha kifo chake papo hapo. 

“Chanzo cha mauaji hayo ni kuwania mali kwani hapo awali marehemu alikutana na watu wanaokadiriwa kuwa watano wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha za moto na mapanga waliokuwa katika harakati za kwenda kuvamia katika duka la Juma Mnyesi mfanyabiashara wa Didia”,ameeleza Kamanda Haule.

“Katika tukio hilo Juma Mnyesi na mke wake aitwaye Mariam Lukuba (47) walijeruhiwa kichwani kwa kitu chenye ncha kali na kisha kuchukuliwa pesa za mauzo ya dukani shilingi milioni 2”,ameongeza Kamanda Haule.

Amesema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga kwa uchunguzi zaidi na majeruhi wamelazwa katika kituo cha afya Bugisi na hali zao zinaendelea vizuri.

Ameongeza kuwa katika eneo la tukio ziliokotwa risasi mbili (Misfire ) na maganda ya risasi 11 za bunduki aina ya AK 47/SAR.

Kamanda Haule anawaomba wananchi wote mkoani Shinyanga kusaidiana na jeshi la polisi kutoa taarifa kuhusiana na waliohusika katika mauaji na uporaji huo ili wakamatwe na sheria ichukue mkondo wake.
Na Kadama Malunde- Malunde1 blog

ANGALIA VIDEO HAPA CHINI KAMANDA WA POLISI MKOA WA SHINYANGA ACP SIMON HAULE AKIWA KATIKA ENEO LA TUKIO
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule akiwa katika kijiji cha Didia baada ya tukio la mauaji kufanyika
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule na wananchi wakiangalia mwili wa marehemu
Mwili wa marehemu ukiwa umefunikwa nguo
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule akiongea na wananchi wa Didia
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule akiwa katika kituo cha afya Bugisi kutembelea majeruhi
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule akiwa katika kituo cha afya Bugisi

Picha kwa hisani ya Ofisi ya RPC SHINYANGA 
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post