Tuesday, January 30, 2018

NABII TITO APANDISHWA KIZIMBANI KWA KUTAKA KUJIUA KWA WEMBE

  Malunde       Tuesday, January 30, 2018
Tito Onesmo Machibya anayejulikana kama 'Nabii' Tito (44) ambaye ni mkazi wa kijiji cha Nong'ona Manispaa ya Dodoma jana Januari 29, 2018 amepandishwa mahakamani katika mahakama ya wilaya kwa shtaka la kutaka kujiua. 


Nabii Tito amepandishwa kizimbani  akidaiwa kutaka kujiua mwishoni mwa wiki jana ambapo alijichana chana na wembe katika baadhi ya maeneo ya mwili wake wakati Jeshi la Polisi likifanya uchunguzi nyumbani kwake. 

Januari 23, 2018 Nabii Titoo alikamatwa na jeshi la polisi akituhumiwa kufanya uchochezi na baadaye alipelekwa kupimwa akili katika hospitali ya wagonjwa wa akili (Mirembe) na kufahamika kuwa mtu huyo alikuwa na matatizo ya akili, hivyo jeshi la polisi liliendelea kumshikilia kwa ajili ya usalama wake na siku jeshi hilo lilipokwenda kufanya uchunguzi nyumbani kwake ndipo alifanya jaribio la kutaka kujiua.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post