MENEJA WA WAKALA WA MAJENGO - TBA AKAMATWA NA POLISI KWA KUSHINDA KUKARABATI MAJENGO YA SHULE KIGOMA | MALUNDE 1 BLOG

Friday, January 5, 2018

MENEJA WA WAKALA WA MAJENGO - TBA AKAMATWA NA POLISI KWA KUSHINDA KUKARABATI MAJENGO YA SHULE KIGOMA

  Malunde       Friday, January 5, 2018
Jeshi la polisi linamshikilia Meneja wa Wakala wa Majengo (TBA), Mhandisi Mgalla Mashaka kwa tuhuma za kushindwa kukarabati Shule ya Sekondari Kigoma.


Meneja huyo alikamatwa akituhumiwa kushindwa kukarabati shule ya sekondari Kigoma kwa wakati licha ya kupewa zaidi ya shilingi milioni mia nne kati ya mia tisa tangu mwezi wa nane mwaka jana.


Mhandisi Mgalla amekamatwa baada ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, kufanya ukaguzi katika shule hiyo ambayo imeanza kupokea takribani wanafunzi elfu moja huku katika miezi mitano ya ukarabati hadi sasa ukarabati wa vyoo, mabweni, maabara na vyumba vya madarasa haujakamilika


Prof. Ndalichako amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa TBA kufika Kigoma kutatua tatizo hilo ili kuepusha maafa yanayoweza kutokea. Kutokana na hali hiyo serikali imeamua kujenga vyoo vya muda ili wanafunzi waweze kuanza masomo wiki ijayo.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post