LOWASSA AKUTANA NA MBOWE KUMPA MREJESHO WA IKULUWaziri mkuu wa zamani Edward Lowassa amekutana na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ili kumpa mrejesho ya alichozungumza na Rais John Magufuli.
Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi na Msemaji wa Lowassa imeeleza kuwa kumekuwa na waraka na taarifa nyingi za kupotosha umma kuhusu ziara ya Lowassa kwenda Ikulu na nyingine zikisemwa zimetoka kwa msemaji wake.
“Taarifa zote hizo siyo kweli na wala siyo rasmi kutoka ofisini kwa Mh Lowassa. Baada ya ziara ile, Mhe Lowassa alikutana na mwenyekiti wa chama chake, Mhe Freeman Mbowe na kumpa mrejesho wa yaliyojiri Ikulu.”
“Kumekuwa na taarifa nyingi kwenye mitandao zikiwemo kufunguliwa kwa akaunti mbalimbali feki , taarifa zote hizo zipuuzwe kwani zina lengo la kupotosha kwa malengo wanayoyajua wapotoshaji hao pamoja na mawakala wao,”
“Taarifa rasmi zitatolewa kwa njia rasmi na watu wenye mamlaka hiyo.poleni kwa usumbufu wote.”
Mapema leo asubuhi Januari 11,2018 katika mtandao wa Twitter kuna account yenye jina la " Edward Ngoyai Lowassa
imepost kuhusu ziara ya Mheshimiwa Edward Lowassa Ikulu hivi karibuni.

Tweet hiyo inasomeka:

Naheshimu Msimamo wa Mwenyekiti wangu baada ya mimi kwenda Ikulu kuonana na Rais Magufuli. Yote aliyoyasema ni malalamiko yetu siku zote lakini mabaya hayawezi kuwa ukuta wa kuzuia mazuri yanayofanywa na serikali hiyo hiyo yasionekane. Tukosoe lakini pia tupongeze


Theme images by rion819. Powered by Blogger.