SUMAYE : WANAOJIUZULU UBUNGE,UDIWANI KWA KUSHAWISHIWA KWA FEDHA NA MADARAKA WAKEMEWE




Waziri mkuu mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Fredrick Sumaye amesema wanajiuzulu ubunge na udiwani kwa kushawishiwa kwa fedha na madaraka wanapaswa kukemewa na watu wote.

Katika mahojiano na kituo cha habari za Azam Two jana Ijumaa Sumaye alisema mwanasiasa anayefanya hivyo ni fisadi mkubwa kwani anachezea fedha za wananchi wanazolipa kama kodi.

"Mtu akijiuzulu kwa sababu za msimamo binafsi hiyo ni sawa lakini akijiuzulu kwa nguvu ya fedha na madaraka tunapaswa wote kukemea,"alisema Sumaye.

Alihoji uhalali wa mbunge kujiuzulu nafasi hiyo akiwa chama fulani na kuitaka tena nafasi hiyo katika chama kingine kwa madai ya kutaka kuwatumikia wananchi wakati hata huko alikojiuzulu alikuwa na uwezo wa kufanya hivyo.

"Mtu kama ni mbunge na aliwaomba kura wananchi ili kuwatumika anapaswa kuwatumikia sio kuhama chama na kutaka tena ubunge kwani mbunge kazi yake ni kuwasemea wananchi sio chama chake," amesema Sumaye.

Na Ephrahim Bahemu, Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527