KATIBU MKUU CHADEMA AWAJIBU WANAODAI AMESHINDWA KUIMUDU NAFASI HIYO

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Vincent Mashinji amesema kuwa yeye yuko tofauti na makatibu wengine wa vyama.


Ameyasema hayo Jijini Dar es salaam wakati akifanya mahojiano na kituo kimoja cha Televisheni, ambapo amesema kila kiongozi huwa na mikakati yake ya kiutendaji.


Amesema kuwa wapo baadhi ya watu wanaosema amepooza, mkimya, hana mikiki mikiki kama walivyo viongozi wengine.


“Ukichanganya majukumu yangu ya kikazi na yale aliyokuwa akifanya Dkt. Slaa unaweza kuharibu mipango ya kitaasisi,” amesema Dkt. Mashinji.


Hata hivyo, amezitaja baadhi ya kazi alizozifanya akiwa Katibu Mkuu kuwa ni pamoja na uandaaji wa Katiba ya Chadema pamoja na miongozo mbalimbali.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.