Tuesday, January 2, 2018

JAMBAZI AUAWA KWA KUPIGWA RISASI AKITAKA KUPIGA POLISI SHINYANGA MWAKA MPYA 2018

  Malunde       Tuesday, January 2, 2018

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule akionesha bastola aliyokutwa nayo Joseph Dogani - Picha na Marco Maduhu- Malunde1 blog
***
Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Joseph Dogani (50) mkazi wa kata ya Ndala Mjini Shinyanga anayedaiwa kuwa ni jambazi ameuawa kwa kupigwa risasi na polisi sehemu mbalimbali za mwili wake akidaiwa kutaka kuwapiga risasi askari polisi. 

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Januari 2,2018,Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule amesema tukio hilo limetokea Januari 1,2018 saa 9:45 alasiri. 

Amesema Joseph Dogani alifariki dunia papo hapo baada ya kupigwa risasi na polisi baada ya marehemu kutaka kuwapiga risasi askari waliokuwa wanamfuatilia. 

“Mtuhumiwa alikuwa akijihusisha na matukio mbalimbali ya mauaji,unyang’anyi wa kutumia silaha na uvunjaji ,alikuwa anatafutwa kuhusiana na tukio la kujeruhi na kumpora mlinzi silaha aina ya shortgun iliyopatikana baada ya kuuawa kwa jambazi mwenzake”,ameeleza Kamanda Haule. 

Kamanda Haule amesema baada ya kupekuliwa alikuwa akiwa na bastola yenye risasi nne ndani ya magazine. 
Na Kadama Malunde- Malunde1 blog
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post