DARAJA LAPOROMOKA NA KUUA WATU 10

Watu kumi na mmoja wamefariki baada ya daraja lililokuwa likijengwa katika maeneo ya Chirajara kuporomoka nchini Colombia.


Maofisa wa Colombia wamesema watu waliofariki ni wafanyakazi wa Kampuni ya ujenzi ambao walikuwa kazini.


Maofisa hao wamesema wafanyakazi hao walikuwa wakishughulika na mfumo wa maji kwenye daraja wakati walipokutwa na umauti kwenye mradi huo uliopo kilomita 95 nje ya Gogota.


Taarifa zaidi zinasema watu tisa walifariki paelpale na mtu wa kumi baada ya kupelekwa katika hospitali ya karibu akiwa na majeraha makubwa.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.