CHADEMA YAPATA PIGO,KIGOGO MWINGINE AHAMIA CCM


Kiongozi mkubwa wa upinzani aliyejiunga na CCM leo ni Muslim Hassanali aliyekuwa mgombea ubunge Ilala kwa tiketi ya Chadema 2015 .Pia alikuwa ni  Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa CHADEMA

Kujiunga kwa Hassanali ni mwendelezo wa mfululizo wa viongozi wa upinzani wakiwemo wabunge na madiwani kuondoka na kujiunga CCM.

Tayari viongozi kadhaa wakiwemo wabunge na wapinzani wamejiunga na CCM wakitokea upinzani kwa sababu tofautitofauti ikiwemo ya kuunga mkono serikali ya Rais John Magufuli.

Kiongozi huyo amepokelewa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula akiwa na viongozi wengine wa CCM katika ukumbi wa Checkpoint Pugu jijini Dar es Salaam. 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments