ANGALIA PICHA ZA TUNDU LISSU ALIVYOWASILI NA KUPOKELEWA JIJINI BRUSSELS UBELGIJI | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, January 7, 2018

ANGALIA PICHA ZA TUNDU LISSU ALIVYOWASILI NA KUPOKELEWA JIJINI BRUSSELS UBELGIJI

  Malunde       Sunday, January 7, 2018
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antipas Lissu amewasili katika uwanja wa ndege jijini Brussels, nchini Ubelgiji ambapo amepelekwa kwa ajili ya awamu ya tatu ya matibabu yake yatakayohusisha mazoezi ya viungo.


Tundu Lissu amewasili jijini hapo akitokea katika Hospitali ya Nairobi, nchini Kenya alikokuwa anapatiwa matibabu kwa muda wa takribani miezi minne sasa, kutokana na kushambuliwa kwa risasi.


Mbunge Tundu Lissu, ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa kambi ya Upinzani Bungeni, alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana, alipokuwa akitokea Bungeni, majira ya saa 7 mchana, karibu na nyumbani kwake Area D, Mjini Dodoma.


Kwa Mujibu wa taarifa ya madaktari waliokuwa wanamtibu, walieleza kuwa jumla ya risasi 16 zilimpata Tundu Lissu mwilini mwake, na wamefanikiwa kuzitoa, isipokuwa moja ambayo iko nyuma ya uti wa mgongo wake.


Tundu Lissu alieleza kuwa wataalamu na madaktari wake walishauri kuwa risasi hiyo ni hatari zaidi kama ikitolewa kuliko ikibaki ndani ya mwili wake, kutokana na eneo ilipokwama.


Picha za Mbunge Tundu lissu alipowasili jijini Brussels kwa ajili ya matibabu zaidi.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post