Picha : SHIRIKA LA TVMC LATOA MSAADA WA MAGURUDUMU YA GARI POLISI SHINYANGA,DC MATIRO APONGEZA

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amelipongeza Shirika la lisilo la kiserikali la The Voice of Marginalized Community (TVMC) linalotoa huduma za kijamii kwa upande wa vijana ,watoto na wanawake na makundi yasiyojiweza la mkoani Shinyanga ambalo linatekeleza mradi wa kupambana na matukio ya ukatili wa kijinsia ndani ya jamii kutokana na kufanya kazi zao kwa ukaribu na serikali katika kumaliza matatizo hayo ili kuwafanya wananchi waiishi salama.


Matiro ametoa pongezi hizo leo Jumatano Desemba 20,2017 wakati Shirika hilo likitoa zawadi ya fedha taslimu shilingi 700,000/= kwa ajili ya kununua magurudumu mawili ya gari la polisi ,ili kuendeleza mapambamo ya kukabiliana na matukio ya ukatili wa kijinsia ambayo bado ni changamoto ndani ya jamii.

Alisema mashirika yawe na mafanikio chanya kwenye miradi yao katika kutatua chgangamoto ndani ya jamii,ni lazima washirikiane kikamilifu na serikali kwa sababu wao ndiyo viongozi wa wananchi na wanawafahamu vizuri.

“Natoa wito kwa mashirika pale mnapokuwa mkitekeleza miradi yenu mshirikiane na Serikali pamoja na kufanya mrejesho kama hili Shirika la TVMC linavyofanya hivi sasa, ili kubaini mlipotoka na muendako je kuna mfanikio,kitendo ambacho kitawafanya kubuni mbinu zingine za kulipunguza tatizo ama kulimaliza kabisa,” alisema Matiro.

Aidha aliyataka mashirika hayo pindi yanaposaidia watoto wanaofanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia yawe yanafuatilia maendeleo yao na siyo kuishia njiani ili kuwasaidia kutimiza ndoto zao pamoja na kuwafunga wahalifu ili liwe fundisho kwa wengine.

Naye mkurugenzi wa Shirikala TVMC Musa Ngangala alisema wameona ni vyema kutoa zawadi ya magurudumu ambayo yatarahisisha utendaji wa kazi kwa jeshi la polisi wakati wa kupambana na vitendo hivyo ya ukatili wa kijinsia ndani ya jamii ili kuwatia nguvuni wahalifu.

Alisema katika changamoto ambazo wanakabiliana nazo pamoja na jamii kutokuwa tayari kutoa ushirikiano wa ushahidi mahakamani, na kumaliza kesi kimya kimya kitendo ambacho kimekuwa kikikwamisha kuwafunga jela watuhumiwa mara baada ya ushahidi usioachashaka kukosekana na hivyo kuachiwa huru.

Aliongeza kuwa katika mrejesho wao ambao wameufanya ndani ya miezi Sita iliyopita, wamebaini matukio ya ukatili wa kijinsia yamepungua ndani ya jamii kutokana na wananchi kuanza kujua madhara yake mara baada ya kupewa elimu na kuyatolea taarifa.

Kwa upande wake Ofisa ustawi wa jamii katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Aisha Omari alisema kutokana na jamii kuwa na uelewa katika mwaka huu 2017 yametolewa taarifa matukio ya ukatili wa kijinsia 62, yakiwemo ya mimba za utotoni,vipigo, na kutelekezwa watoto.

Alisema baadhi ya kesi hizo zilifanyiwa suluhu hasa za vipigo, huku zingine zikiendelea mahakamani na kuitaka jamii iachane na tabia ya kumaliza kesi kimya kimya na kuhakikisha wanahudhuria mahakamani ili watuhumiwa waweze kufungwa na kutoa mfano kwa wengine ili kuogopa kuendelea kufanya ukatili huo.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro (kulia) akimkabidhi pesa taslimu Shilingi 700,000/= Mkuu wa Jeshi la polisi wilaya ya Shinyanga Cloud Kanyorota ambazo zimetolewa na Shirika la TVMC kwa ajili ya kununua magurudumu mawili ya gari la jeshi hilo ili kupambana na matukio ya ukatili wa kijinsia - Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro (kulia) akimkabidhi pesa taslimu Shilingi 700,000/= mkuu wa jeshi la polisi wilaya ya Shinyanga Cloud Kanyorota zilizotolewa na TVMC
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiyasisitiza mashirika na taasisi mbalimbali kufanya kazi kwa ukaribu na serikali pamoja na kuleta matokeo chanya kwenye miradi yao ndani ya jamii
Mkurugenzi wa Shirika la TVMC Mussa Ngangala ,akielezea namna wanavyoshirikiana na serikali kutatua matatizo ya ukatili wa kinjisia na kuamua kutoa zawadi ya magurudumu mawili kwa ajili ya gari la jeshi la polisi ili kuendeleza mapambano ya kukabiliana na matukio ya ukatili wa kijinsia na kuwatia nguvuni wahalifu.
Mkurugenzi wa Shirika la TVMC Mussa Ngangala  akizungumza
Afisa Mtendaji wa kata ya Usanda Emmanuel Maduhu akielezea namna elimu ya ukatili wa kijinsia ndani ya jamii ilivyoleta mafanikio na kupunguza matukio hayo
Ofisa Ustawi wa jamii wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Aisha Omari akitoa taarifa kuwa baada ya elimu kupenya kwa wananchi ipasavyo matukio ya ukatili wa kijinsia yaliyotolewa taarifa ni 62 mengine ni ya vipigo vya wanafamilia na yametatuliwa kwa suluhu huku mengine ya mimba,ubakaji, kesi zake zikiwa bado mahakamani
Msaidizi wa dawati la Jinsia na watoto wa Jeshi la polisi Vivian Zabron akielezea namna kesi za ukatili zilivyopungua kwenye dawati hilo tofauti na nyuma kutokana na elimu kuendelea kutolewa ndani ya jamii na kudai bado matukio ya vipigo kwa wanafamilia ndiyo changamoto
Mhadhiri wa Chuo cha Mipango ambaye pia ni mtaalamu wa Social Demograph ,Kwalu Samwel Dede aliyeshiriki kwenye mrejesho wa mradi huo wa ukatili kwa kijinsia na utolewaji wa fedha za magurudumu mawili ya gari la polisi, aliwaasa viongozi wa serikali na mashirika washikamane kufanya kazi kwa pamoja ndipo watafanikiwa dhima yao ya kutokomeza vitendo hivyo vya ukatili ndani ya jamii
Washiriki wakiwa kwenye kikao hicho wakisikiliza na kujadili namna ya kupambana na matukio hayo ya ukatili wa kijinsia ndani ya jamii, wakiwamo maofisa watendaji wa Kata, Vijiji, maofisa maendeleo na dawati la jinsia la Jeshi la Polisi.
Washiriki wakiwa ukumbini
Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527