WATANZANIA 900,000 WANATUMIA DAWA ZA KUFUBAZA MAKALI YA UKIMWIWatoto 10,000 wanaozaliwa Tanzania wana maambukizo ya Ukimwi huku Watanzania 900,000 wakiendelea kutumia dawa za kufubaza makali ya ukimwi.


Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu wakati akifungua majengo ya chuo cha uuguzi cha Mirembe mjini Dodoma.


Waziri Mwalimu amesema kiwango hicho ni kikubwa ambacho kinapaswa kupunguzwa kwa juhudi za haraka kwani lengo lake ni kuona watoto wote wanazaliwa bila maambukizo.


Wakati huo Mwalimu amekiri kuwa kiwango cha fedha zinazotolewa na wafadhili kwa ajili ya kupambana na malaria zinatumika kwa matangazo ambayo mengi hayana tija.


Waziri amemwagiza Katibu Mkuu kushughulikia matatizo na mapungufu katika vyuo vya wauguzi ili viweze kutoa watu wenye ujuzi wa hali ya juu katika kuwahudumia Watanzania.

Na Habel Chidawali, Mwananchi
Theme images by rion819. Powered by Blogger.