MBUNGE WA CHADEMA AZUA GUMZO, AITISHA MKUTANO WA WAANDISHI WA HABARI NA KUSHINDWA KUWAELEZA ALICHOWAITIA

Mbunge wa viti maalumu kwa tiketi ya CHADEMA kutoka Mkoa wa Geita, Upendo Peneza leo Desemba 15, 2017, ameitisha mkutano na Waandishi wa Habari, Mkutano ambao umeleta gumzo mitandaoni kutokana na wimbi la Wabunge wa Vyama vya Upinzani kukimbilia CCM.

Mhe. Peneza ameitisha mkutano huo bila kueleza nini hasa anachoenda kuzungumzia kitu ambacho kimeleta maswali mengi kwa wafuasi wa CHADEMA nchini Tanzania.

Mkutano huo unajiri ikiwa ni siku moja tu imepita tangu Mbunge wa jimbo la Siha, Mhe. Godwin Mollel kutangaza kukihama chama hicho na kuhamia CCM.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.