WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI WAKAMATWA NA SIMU KWENYE CHUMBA CHA MTIHANI WA TAIFA


Wanafunzi wawili wa Shule ya Sekondari Lady of Mercy iliyopo eneo la Shauri Moyo, Nairobi wamekutwa na simu kwenye chumba cha mtihani, hivyo watajibu mashitaka mahakamani.

Walitarajiwa kupandishwa kizimbani siku ya Jumatatu Novemba 13,2017 katika Mahakama ya Makadara kujibu mashtaka ya udanganyifu kwenye mtihani wa Cheti cha Elimu ya Sekondari (KCSE). Waziri wa Elimu nchini Kenya, Fred Matangi amesema jana kuwa, wanafunzi hao hawataendelea kufanya mitihani na watashtakiwa mahakamani.

Waziri Matiangi alionya kuwa, Serikali itafuta usajili wa shule binafsi zitakazobainika kujaribu kufanya udanganyifu kwenye mitihani. Taarifa ya kiongozi huyo imesema, mtu au taasisi inayojaribu kufanya udanganyifu kwenye mitihani inayoendelea hatavumuliwa.

Kwenye taarifa hiyo alisema, Wizara ya Elimu na Tume ya Walimu itachukua hatua za kinidhamu dhidi ya wasimamizi wa vituo au maofisa watakaohusika kutaka kufanya udanganyifu. Jana asubuhi Waziri Matiangi alishuhudia kuanza kwa mtihani wa pili katika Shule ya Juu ya Sekondari Aga Khan.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.