Picha : DC SHINYANGA AZINDUA MRADI WA MTOTO MWEREVU UNAOTEKELEZWA NA TVMC


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amezindua mradi wa Mtoto Mwerevu unaolenga kuwapatia lishe watoto wenye umri wa siku 1000 katika kata tano za manispaa ya Shinyanga ambazo ni Kizumbi,Ibadakuli, Chamaguha,Mwawaza na Mwamalili.

Mradi huo utakaodumu kwa muda wa miaka minne unatekelezwa na Shirika la lisilo la kiserikali la The Voice of Marginalized Community (TVMC) linalotoa huduma za kijamii kwa upande wa vijana ,watoto na wanawake na makundi yasiyojiweza.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika leo Jumatatu Novemba 13,2017 katika ukumbi wa Diamond Field Hotel mjini Shinyanga,Matiro alilitaka shirika la TVMC kuwafikia walengwa ili kupunguza idadi ya watoto wenye udumavu katika jamii.

“Nawapongeza kwa kuanzisha mradi huu,mnachotakiwa kuzingatia ni kushirikisha walengwa wote wanaotakiwa ili mradi huu uwe na mafanikio mazuri,shirikisheni viongozi wa mitaa na kata kwani wao ndiyo wapo karibu zaidi na jamii”,alisema Matiro.

Akielezea kuhusu mradi huo, Mkurugenzi wa TVMC,Mussa Jonas Ngangala alisema lengo la mradi wa Mtoto Mwerevu ni kupunguza udumavu kwa watoto wenye umri wa siku 1000 katika kata tano za manispaa ya Shinyanga.

“Baada ya kufanya utafiti,tulibaini kuwa kati ya kata 17 za manispaa ya Shinyanga,tulibaini kuwa kata tano za Kizumbi,Ibadakuli, Chamaguha,Mwawaza na Mwamalili kuna idadi kubwa ya watoto waliodumaa kutokana na kukosa lishe bora”,alisema Ngangala.

“Tumepanga kutekeleza mradi huu kwa kipindi cha miaka minne lakini tutaanza kwa majaribio ya mwaka mmoja na kama kutakuwa na mafanikio basi tutaendelea kutekeleza mradi huu ambao walengwa wakuu ni akina mama wajawazito na akina mama wanaonyonyesha”,alieleza Ngangala.

Alisema mojawapo ya mbinu watakazotumia kufanikisha mradi huo kuwa ni kuhamasisha akina mama wajawazito na wanaonyonyesha kutumia lishe bora kwa kuzingatia makundi matano ya vyakula.

Ngangala aliyataja makundi matano muhimu ya chakula katika kupambana na udumavu kwa watoto kuwa ni nafaka,mizizi na ndizi, vyakula jamii ya nyama na mikunde,mboga mboga,matunda na sukari,asali na mafuta.

Aliongeza kuwa ili kufanikisha mradi huo watafanya kazi zaidi na vikundi mbalimbali katika jamii ambavyo vitakuwa mstari wa mbele kuhamasisha namna ya kunyonyesha,jinsi ya kuandaa chakula cha mtoto,faida za kunawa,kilimo cha bustani ya mboga mboga pamoja na ufugaji kwa ajili ya lishe bora.

Uzinduzi wa mradi wa mtoto mwerevu umehudhuriwa na maafisa maendeleo ya jamii manispaa ya Shinyanga, ,mwakilishi wa mkurugenzi wa manipaa,maafisa kilimo kata na maafisa watendaji wa kata na mitaa.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza katika ukumbi wa Diamond Field Hotel mjini Shinyanga wakati wa kuzindua mradi wa Mtoto Mwerevu unaotekelezwa na shirika la TVMC-Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisisitiza umuhimu wa watekelezaji wa mradi wa mtoto mwerevu kushirikisha walengwa katika jamii
Mkurugenzi wa Shirika la lisilo la kiserikali la The Voice of Marginalized Community (TVMC) ,Mussa Jonas Ngangala akielezea kuhusu mradi wa "Mtoto Mwerevu"
Mkurugenzi wa TVMC) Mussa Jonas Ngangala akielezea malengo ya mradi wa Mtoto Mwerevu
Wadau walioshiriki katika uzinduzi wa mradi wa Mtoto Mwerevu wakiwa ukumbini
Mkurugenzi wa TVMC) Mussa Jonas Ngangala akielezea kuhusu makundi matano muhimu ya chakula katika kupambana na udumavu kwa watoto ambayo ni kundi la nafaka,mizizi na ndizi, vyakula jamii ya nyama na mikunde,mboga mboga,matunda na sukari,asali na mafuta.
Picha ikionesha makundi muhimu ya chakula
Wadau wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea wakati wa uzinduzi wa mradi wa mtoto mwerevu
Wadau wakiwa ukumbini
Wadau wakiwa ukumbini
Wadau wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea wakati wa uzinduzi wa mradi wa mtoto mwerevu
Uzinduzi unaendelea
Wadau wakiwa ukumbini
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527