MTANDAO WA UTEPE MWEUPE WATOA ELIMU YA VIFO VITOKANAVYO NA UZAZI KWA AKINA MAMA NA WATOTO WACHANGA KIJIJI CHA MAORE SAME


Mratibu wa Mtandao wa Utepe Mweupe kitaifa (The White
Ribbon Alliance ) Rose Mlay akizungumza na wananchi katika kijiji cha Maore wilayani Same mkoani Kilimanjaro wakati wa mkutanowa hadhara ulioandaliwa na Taasisi ya Utepe mweupe (White Ribbon) kujadili vifo vya akina mama wajawazito na
watoto wachanga.

Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Maore wilayani Same akifuatilia kwa makini majadiliano yaliyokuwa yakiendelea kuhusu vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga.
Mganga Mkuu wa wilaya ya Same,Dkt Godfrey Andrew akizungumza wakati wa mkutano na wananchi ulioandaliwa na Mtandao wa Utepe Mweupe (White Ribbon) kujadili vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga.

Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Maore wilayani Same akifuatilia kwa makini majadiliano yaliyokuwa yakiendelea kuhusu vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga.
Mkutano ukiendelea katika jengo la Mahakama lililopo katika kijiji cha Maore wilayani Same.

Baadhi ya kina mama wakiwa na watoto wao katika mkutano huo.



Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Maore wilayani Same wakichangia wakati wa mkutano uliondaliwa na Mtandao wa White Ribbon kuhusu vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga .

***
WANANCHI katika kijiji cha Maore wilayani Same mkoa wa
Kilimanjaro,wamesema tatizo la vifo vya akina mama vitokanavyo na uzazi pamoja na watoto wachanga vinachangiwa na upungufu wa watumishi katika zahanati ya kijiji pamoja na ufinyu wa wodi ya wazazi iliyopo.

Wakitoa maoni yao katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na
Taasisi ya Utepe mweupe (White Ribbon) kujadili vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga katika kijiji cha Maore wilayani Same wananchi hao wameiomba serikali kuangalia namna ya kutatua changamoto hizo.

Mbali na changamoto hizo wakazi wa Maore wameeleza pia
changamoto kubwa inayowakabili wanafunzi wa kike kupata ujauzito pindi wawapo shuleni kuna changiwa na wazazi kushindwa kuwaeleza ukweli watoto wao kuhusu kuanza mahusiano wawapo shuleni.

Mganga Mkuu wa wilaya ya Same ,Dkt Godfrey Andrew amesema vifo vya akina mama vitokanavyo na uzazi pamoja na watoto wachanga vimepungua wilayani Same hadi kufikia 15 mwaka
huu ukilinganisha na vifo 60 vilivyotokea katika miaka miwili iliyopita ya 2015 na 2016 huku akibainisha mikakati iliyopo ya kupambana na changamoto za upungufu wa watumishi.

Mratibu wa Mtandao wa Utepe Mweupe kitaifa (The White Ribbon Alliance ) Rose Mlay amesema kuwekeza kwa mama mjauzito kunachangia kuzaliwa kwa kijana mwenye afya njema atakayechangia katika ukuaji wa uchumi wa nchi na kulea maendeleo.

Same ni mojawapo ya wilaya saba zilizoko katika mkoa wa
Kilimanjaro zinazokabiliwa na changamoto ya vifo vya akina mama wajawazito vitokanavyo na uzazi huku sababu ya vifo hivyo kwa kina mama ikielezwa kuwa ni kifafa cha mimba,kupasuka kwa mji wa mimba na kutokwa na damu nyingi.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527