ACACIA WASEMA HAWANA UWEZO WA KULIPA DOLA MILIONI 300 KWA SERIKALI YA TANZANIA

Kampuni ya uchimbaji madini, Acacia (Acacia Mining) imefunguka na kusema kuwa haina uwezo wa kulipa dollar milioni 300 kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kutatua mgogoro wa kodi.


Akiongea jana Oktoba 20, 2017 kwa njia ya simu na chombo cha habari cha Kimataifa cha Uingereza (Reuters) Afisa wa Fedha wa Acacia, Andrew Wray kampuni hiyo haina uwezo wa kulipa fedha hizo kwa serikali ya Tanzania.


Washirika wakubwa wa Acacia, Barrick Gold siku ya juzi Oktoba 19 walikubalina na serikali ya Tanzania kuwa watalipa dollar milioni 300 kwa serikali ya Tanzania pamoja na kugawana mapato yanayotokana na shughuli za uchimbaji wa madini nchini.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post