Video: UHURU KENYATTA AMPA ONYO RAILA ODINGA..AMTAKA ASAHAU KUHUSU TUME MPYA YA UCHAGUZI


Aliyekuwa Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta amefunguka na kutoa onyo kwa mpinzani wake Raila Odinga kuwa asahu kuhusu tume mpya ya uchaguzi lakini pia amemtaka Jaji Mkuu wa Kenya David Maraga kutoingilia kwani wao wameheshimu maamuzi ya mahakama.

Uhuru Kenyatta amesema chama chake cha Jubilee kipo tayari kwa uchaguzi huo wa marudio na sasa wanasubiri Tume ya Uchaguzi nchini Kenya IEBC iweze kutangaza siku ya uchaguzi na wanaiomba itangaze siku hiyo haraka.

Aidha Uhuru Kenyatta amesema kuwa wapinzani hao hawana haja ya uchaguzi bali ni watu ambao wanataka serikali ya mseto kitu ambacho yeye hawezi kukiruhusu hata kidogo.

Mahakama ya juu nchini Kenya Septemba 1, 2017 ilifuta matokeo ya Urais nchini Kenya na kuamuru kuwa uchaguzi mpya ufanyike katika nafasi ya Urais kutokana na mahakama hiyo kubaini baadhi ya mapungufu wakati wa utoaji wa matokeo hayo ya uchaguzi uliofanyika Agosti 8, 2017.

Mtazame hapa Uhuru Kenyatta akifunguka mengi zaidi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post