Picha & Video: TCRA YAKUTANA NA BLOGGERS..YAZINDUA KAMPENI YA 'USINITUMIE,SITAKI,SIMTUMII MWINGINE,NITAKURIPOTI'

Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jones Kilimbe akifungua rasmi warsha ya vyombo vya Habari Mtandaoni iliyowahusisha Blogu na 'Online Tv' katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa J.K Nyerere Jijini Dar es salaam.
Bw. Thadeus Lingo kutoka TCRA akiendesha mada kuhusu Matumizi Salama ya Mitandao ya Kijamii 
Mwakilishi wa Chama cha wamiliki wa Blogu Tanzania(TBN) Bw. Maxence Melo akiwasilisha mada juu ya Maudhui ya Mtandaoni na Changamoto zake.
Mratibu Msaidizi wa Polisi Joshua Mwangasa akitoa mada juu ya Hali ya Usalama Mtandaoni
Mzee Abdul Ngarawa Mjumbe wa Kamati ya Maudhui kutoka TCRA akitoa neno la Busara wakati wa warsha hiyo ambapo alisisitiza kuzingatia uzalendo umuhimu wa kutazama utu na staha ya mtu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi James Kilaba (Kushoto) akiongoza majadiliano kwa ujumla ambapo wadau walichangia mawazo na kuuliza maswali mbalimbali 
Bwana Daniel Mbega Mmiliki wa Blogu ya Maendeleo Vijijini akichangia mawazo yake wakati wa warsha hiyo
Bw. William Malecela Maarufu kwa jina la Le Mutuz mmiliki Blogu ya Wananchi na Le Mutuz Tv Online akichangia mambo mbalimbali na kutoa maoni yake wakati wa Warsha hiyo
Mwenyekiti wa Chama cha wamiliki wa Blogu Tanzania(TBN) Bw. Joachim Mushi (kulia) akitoa neno la Shukrani kwa niaba ya waendeshaji wote wa mitandao/blogs kwa TCRA kuendesha warsha hiyo 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi James Kilaba pamoja na wadau wengine wakizindua Rasmi Kampeni ya kusisitiza matumizi bora ya Mitandao ya Kijamii awamu ya Pili ambapo Kauli mbiu inasema "Usinitumie Sitaki na Simtumii Mwengine Nitakuripoti"
Baada ya uzinduzi wa Kampeni hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA Bi. ValerieNdeneingo-Sia Msoka akitoa neno la kufunga wakati wa Warsha hiyo.

Wadau mbalimbali wakiwa katika warsha hiyo

Picha zote na Fredy Njeje/ Blogs za Mikoa Tanzania


**************Serikali ya Awamu ya Tano kupitia Mamlaka ya Mawasiliano nchini(TCRA) imetia nia kuboresha mawasilianokwa umma hasa katika matumizi ya mitandao ya kijamii ili kuwawezesha watanzaniakupata elimu bora ya maendeleo na kujenga uchumi ulio bora.


Haya yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi wa Mamlaka hiyo Dkt. Jonas Kilimbe alipokua akihutubia hadhara yawamiliki wa vyombo vya habari mtandaoni (blogu na Online TV) katika uzinduzi wa kampeni ya awamu ya pili ya “kusisitiza matumizi bora ya mitandao ya kijamii” iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere.

Katika hafla hiyo, Dkt. Kilimbe alisema kuwa kwa sasa teknolojia ya mtandao inakua kwa kasi kwa hiyo huduma za habari zinapatikana kila sehemu kwa njia ya mtandao na kufanya matumizi ya mitandao kuwa makubwa.

“Sekta ya mawasiliano kwa umma imepiga hatua kubwa sana duniani kwa sasa, kwa kiasi kikubwa mtandao unachangia kuwepo kwa habari nyingi. Tanzania inajumla ya televisheni za mitadaoni
zipatazo 50 pamoja na blogu 150 ambazo zote zinatoa taarifa kwa wananchi, hii inaashiria kuwa mawasiliano kwa umma yamehamia zaidi kwenye mtandao”, alisema Dkt.Kilimbe.

Aidha Dkt.Kilimbe alisema kuwa sekta hii inapaswa kuangaliwa zaidi kwani ni sekta muhimu kwa ujenzi wa Taifa na kuwaasa vijana kutumia vizuri teknolojia hiyo kwa kujielimisha kuhusiana na masuala ya maendeleo kuliko kutumia vibaya mitandao hiyo.

“Tuna jukumu zito na ni kubwa kwa sababu sekta hii ya mawasiliano imeshikiria kila kitu na tasnia ya habari ina nguvu kubwa sana kwa kuleta elimu ya maendeleo kwa wananchi kwa hiyowaandishi mitandaoni tumieni weledi 
mkubwa kwa habari za maendeleo”, alisisitiza Dkt. Kilimbe.

Dkt.Kilimbe alisema katika matumizi ya teknolojia hii mpya yanapaswa kuzingatiwa kwa ajili ya ujenzi wa taifa hasa kwa wale
wanaotumia vizuri mitandao ya kijamii inawapa elimu kubwa ya maendeleo.

Aidha Dkt. Kilimbe amekishukuru chama cha wamiliki wa blogu na televisheni mtandaoni(TBN) kwa kuleta umoja na kuzingatia maadili na weledi wa umiliki wa vyombo hivyo kwa kuwahabarisha wananchi.

Naye mtoa mada na mwakilishi kutoka TCRA Bw. Thadeus Lingo alisisitiza usalama wa matumizi ya mtandao akisema kuwa idadi ya watumiaji wa mitandao imeongezeka duniani kuanzia
Julai 1, 2017 na kufikia bilioni 3.8 huku kati ya hao bilioni 3.4 ambayo ni sawa na asilimia 92 ni watumiajia wa mitandao ya kijamii hali iliyosababisha kuongezeka kwa vyombo vya habari kuhamia mtandaoni, kwa hiyo weledi unahitajika
katika kuhabarisha umma kwa njia hii.


Na Paschal Dotto-MAELEZO.

Nimekuwekea hapo Video fupi ya Uzinduzi wa Kampeni hiyo hapa chini unaweza kuitazama.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.